Mshambuliaji nyota wa klabu ya Atletico Madrid Luis Suarez amevunja ukimya baada ya kuhusishwa na kuhamia kwenye klabu ya Aston Villa inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza lakini siku ya jana alitumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii kuaga mashabiki na wafanyakazi wa klabu hiyo lakini alishindwa kusema ni wapi atacheza kwa msimu ujao

Aston Villa wamehusishwa katika kuwania saini ya mshambuliaji Luis Suarez kwenye uhamisho huru wa majira ya kiangazi, baada mkataba wake kuisha na klabu ya Atletico Madrid mwishoni mwa msimu huu.

Luis Suarez

Luis Suarez ambaye siku ya jumapili baada ya kucheza mchezo wake wa mwisho kwenye klabu hiyo alitumia ukurusa wake wa Instagram aliandika, “moyoni nawashukuru mshabiki mmoja mmoja, mfanyakazi mmoja mmoja wa @atleticodemadrid kwa upendo wao  walionionesha, siku hadi siku na familia yangu ambayo muda wote wamekuwa upande wangu.

“Ninaondoka na upendo wa hii klabu, baada ya kushindwa kufurahia msimu uliosha. Nitaiweka Atletico moyoni mwangu.”

Luis Suarez mwenye miaka 35 anajiandaa kuondoka kwenye ligi kuu ya Hispania kwenye majira ya kiangazi, baada ya mkataba wake kuisha na klabu ya Aston Villa inajiandaa kumpa offa ambayo itamvutia, ili aweze kukubali kurudi kwenye ligi kuu ya Uingereza baada ya uhamisho wa mwezi January kushindikana.

Kocha wa klabu wa Aston Villa Steven Gerrard alishawai kucheza na Luis Suarez kwenye klabu ya Liverpool kuanzia mwaka 2010 hadi 2014.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa