Luiz Diaz Kukosekana Leo Dhidi ya Nottingham

Winga wa klabu ya Liverpool raia wa kimataifa wa Colombia Luiz Diaz atakosekana tena leo katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza kati ya klabu yake dhidi ya Nottingham Forest.

Luiz Diaz hakosekani katika mchezo wa leo kutokana na majeraha au adhabu ya kadi, Bali kinachomkosesha winga huyo mchezo huu ni matatizo ya kifamilia ambapo familia yake imetekwa nchini kwao Colombia.Luiz DiazMama mzazi wa winga huyo aliokolewa na polisi nchini Colombia lakini mpaka sasa familia yake inashikiliwa na magenge ya kihuni nchini humo, Hivo kumlazimu mchezaji huyo kuendelea kufatilia uokozi wa familia yake.

Mpaka sasa hakuna taarifa za kupatikana kwa baba wa mchezaji huyo ambaye ni miongoni mwa wanafamilia waliotekwa na magenge ya kihuni nchini Colombia, Lakini polisi nchini humo bado wanaendelea na uchunguzi vilevile.Luiz DiazWinga Luiz Diaz kukosekana kwenye kikosi cha Liverpool ni pigo kwani ni moja ya wachezaji muhimu klabuni hapo kwasasa, Lakini maisha ya familia yake ni muhimu zaidi na ndio sababu Liverpool wamemuacha akafatilie mustakabali wa maisha ya familia yake kwanza.

 

Acha ujumbe