Mshambuliaji wa Chelsea, Romelu Lukaku anataka kurejea katika klabu yake ya zamani ya Inter Milan endapo klabu hizo zitafikia makubaliano.

Inter Milan wameweka wazi hawawezi kumsajili mshambuliaji huyo kwa mkataba wa kudumu kwasasa, na uamuzi wa mwisho uko kwa Boss mpya wa Chelsea ambaye ameinunua klabu hiyo.

 

Lukaku, Lukaku Adhamiria Kurejea Inter Milan., Meridianbet

Mwanasheria wa Romelu atakutana na Inter Milan siku ya Jumanne kuangalia uwezekano wa mshambuliaji huyo kurejea Itali kulingana na Sky Italy.

Lukaku, 29 alijiunga na Chelsea kwa dau la rekodi ya klabu la £97.5m katika majira ya kiangazi msimu uliopita na aliweka wazi nia yake ya kurejea Inter katika mahojiano yaliyozua mjadala na Sky Italy.

Mtendaji Mkuu wa Inter, Giuseppe Marotta amesema hawana haraka kuhusu kumrejesha Lukaku lakini wanabaki kumuhitaji zaidi katika dirisha hili la kiangazi.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa