Nyota wa Inter Romelu Lukaku anasema kuwa angejiweka ‘katika washambuliaji watano bora ulimwenguni kwa hivi sasa’ katika kuelezea namna makocha walivyombadilisha kimtazamo kwa mchezo huo.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alizungumza na waandishi wa habari katika jarida la michezo la Voetbal Magazine la Ubelgiji juu ya soka lake la kulipwa na mafanikio ya sasa huko San Siro.
Lukaku -ambaye anasisitiza kuwa kila anapoingia uwanjani lengo lake huwa moja tu, ushindi – anaamini mtazamo wake huu ni muhimu zaidi nchini Italia, na ni sehemu ya mafanikio yake.

Staa huyu wa zamani wa Manchester United amebainisha kuwa kuna tofauti kubwa sana ya soka la Italia na Uingereza, na Italia anafanya zaidi kile wanachomuhitaji afanye, ndicho anachozingatia na kwa namna yeyote hataki kutengeneza mazingira ya kumkwamisha juu ya hilo.
“Kwa miezi mitano iliyopita, ningejiweka katika orodha ya washambuliaji watano bora ulimwenguni hivi sasa, Sitaki kuandaa orodha ya wengine, lakini najiona niko ndani.” – Romelu Lukaku
Nyota huyu alisema kuwa makocha wamembadilisha sana kimtazamo na namna anavyoliona soka, na vile anavyofanya kazi.
Mchezaji huyo wa miaka 27 amecheka na nyavu mara 15 katika mechi 18 za mashindano ya Inter msimu huu, pamoja na kutoa asisti mbili.
VUNA SHEA YAKO YA 230,000,000TSH NA UFURAHIE MSIMU HUU WA SIKUKUU!!!
Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, jiwekee nafasi ya kupata shea yako ya 230,000,000Tsh kupitia mchezo wa Secret Santa. Hakika hutojutia kufurahia msimu huu wa sikukuu ukiwa katika nyumba ya mabingwa ya Meridiabet. Unasubiri nini?




warda
Alipoa sana bora kaja juu
Tatu
Lukaku anajituma sana
Fatina mfingi
Endelea kujituma lukaku utafika mbali
Rahmal
Lukaku anafanya vizuli
Sarah
Lukaku azidi kujituma atafika mbali
Hopemwaikuka
Hata m nakubal
Caroline
Lukaku yupo vizuri
Saupha mohamed
Ni kweli kabsaa yupo viziri
Dorophina
Lukaku yupo vizuri anaweza akawa amefikia hatua iyo
Zahara omary
Lukaku yupo vizur
Lydia Emmanuel Magoti
Namkubali Lukaku anajua
Sania
Kaza buti Lukaku ili ndoto yako itimie