Mshambuliaji wa klabu ya Inter Milan Romelu Lukaku ambaye anatarajiwa kurejea katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya klabu Victoria Plzen ambao Inter watakua nyumbani ameeleza kocha wa klabu hiyo Simeone Inzaghi.
Lukaku ambae alifunga mabao 24 wakati Inter Milan ikiwa bingwa wa ligi kuu ya Italia maarufu kama Serie A alitarajiwa kua muhimu zaidi wakati anarejea klabuni hapo akitokea klabu ya Chelsea kwa mkopo wa msimu mzima.
Jeraha la paja limemfanya mchezaji huyo kukaa nje ya uwanja toka mwezi Agosti mwaka huu na sasa amepata nafuu kuliko ilivyotarajiwa mwanzo na anarejea hivi karibuni.
Mchezaji huyo atarejea katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Victoria Plzen ambapo mchezo huo ndo utaamua hatma ya klabu hiyo ya ligi ya mabingwa ulaya lakini atakosekana katika mchezo wa Serie A utakaopigwa jumamosi hii.
“Amekua akifanya mazoezi kwenye kundi kwa siku mbili. Anapaswa kurejesha hali yake, Lakini ana ari kubwa baada ya muda mrefu sana ameshinda jeraha” Alisema kocha Inzaghi akimuongelea Lukaku.

