Klabu ya Inter Milan imefikia makubaliano na klabu ya Chelsea kumrejesha mshambuliaji wa Ubelgiji, Romelu Lukaku kwa mkopo wa mwaka mmoja baada ya kushindwa kufanya vizuri tangu aliporejea Stamford Bridge.

Milan wanatarajiwa kulipa kiasi cha Euro milioni 8 pamoja na bonasi ya Euro milioni 4 katika kipindi chote cha mkopo akiwa Italia, baada ya bosi mpya wa klabu hiyo kupitisha mkopo huo.

 

Romelu Lukaku

Lukaku, 29 anatarajiwa kufanya vipimo vya afya mapema wiki ijayo nchini Italia katika hitimisho la kurejea kwenye dimba la San Siro kabla ya msimu mpya kuanza.

Akiwa Chelsea, Romelu Lukaku amecheza jumla ya mechi 26 katika mashindano yote kutokana na majeraha akifanikiwa kufunga magoli 8 pekee katika kipindi cha msimu mzima aliodumu EPL.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa