Luke Shaw Arejea Mazoezini Man United

Beki wa kushoto wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Uingereza Luke Shaw amefanikiwa kurejea kwenye kikosi cha klabu hiyo baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Beki huyo ambaye amekua akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara amerejea kwenye timu tangu mwishoni mwa msimu uliomalizika, Kwani msimu beki huyo hakufanikiwa kumaliza msimu kwakua alikua akisumbuliwa na majeraha ambayo yameendelea kumuandama mpaka msimu huu.luke shawLuke Shaw alipona majeraha yake lakini hakuweza kuitumikia klabu yake badala yake akaitwa timu ya taifa kwenye michuano ya Euro iliyofanyika mwezi wa sita mpaka wa saba, Ambapo baada ya mixchuano hiyo kumalizika aliripotiwa kupata majeraha tena ambayo yamemueka nje kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu.

Kurejea kwa beki Luke Shaw kwenye kikosi kunaendelea kuleta matumaini kwa klabu hiyo na kwa kocha mpya ambaye anakuja klabuni hapo Ruben Amorim, Kwani kocha huyo atakuta wachezaji karibia wote wamepona majeraha yao mabapo hivi karibuni Mason Mount amerejea, Leny Yoro, huku Kobbie Mainoo na Harry Maguire wakitarajiwa kurejea hivi karibuni.

Acha ujumbe