Mlinzi wa Man United Luke Shaw ameamua kuwaboa mashabiki wa Liverpool kwa kutaka msimu huu wa ligi ubatilishwe na Liverpool wasipewe taji la Ligi Kuu ya Uingereza.
Inakumbukwa kuwa msimu huu umesimama kwa sababu ya janga la Virusi vya Corona ambavyo limekwamisha shughuli nyingi karibu duniani kwote kwa sasa.
Kuna mechi 92 ambazo bado zimebakia kuchezwa kwa msimu huu, huku kukiwa na wazo la kumaliza kwa mfumo kama wa Kombe la Dunia ili mechi ziishe kwa pamoja. Mipango ya kumalizia michuano hii imebaki kuwa ni kitendawili kufuatia nchi nyingi kuwa bado kwenye zuio la kupokea wageni au kusafiri na kutoka nje.
Liverpool wamefanya vyema sana msimu huu na wanatarajiwa wangelichukua taji hili la Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu. Lakini kwa mujibu wa Shaw, yeye anaona kama rekodi ya Liverpool ingevunjwa tuu huku msimu msimu ukibatilishwa kwa sababu ya changamoto hii ya dunia.
Huu ni ujumbe mzito sana kwa Shaw kuutuma kwa mashabiki wa Liverpool ambao wanatarajia msumu huu kiuisha vyema kwa upande wao.
Hata hivyo, taarifa zinataja kuwa mabosi wa Ligi Kuu Uingereza wapo kwenye mazungumzo juu ya uwezekano na namna ya kurejesha michuano hii ili kumalizia sehemu ya ligi iliyosalia.