Kwa sasa Zidane ameanza kibarua chake kwa awamu nyingine tena kama kocha wa kikosi hicho cha matajiri wa Hispania. Hajataka kabisa kulaza mambo, ameanza vuguvugu la usajili mapema ili kurejesha nguvu mpya kwenye kikosi chao hicho ambacho kimepotea kwenye upeo wa kisoka.
Bila kukawia tayari amekwishaanza na upande wa safu ya ulinzi kwa kumsajili mlinzi raia wa Brazil na mchezaji wa klabu ya FC Porto, Eder Militao kwa uhamisho unaokadiriwa kufika £43m ikiwa ni kwa mkataba wa miaka sita kutumikia klabu hiyo. Uchaguzi huo ni mwafaka kabisa na unaweza kukipa matunda kikosi hicho bila wasiwasi wowote.
Ni maamuzi sahihi kuanza kuhudumia safu ya ulinzi kutokana na mwenendo wake wa kuruhusu magoli mengi msimu huu na kuonekana kama safu ambayo imekaa muda mrefu na kuanza kupoteza ubunifu wa ndani ikiwa ni kwa kipindi kirefu sana wamehudumu pamoja katika viunga hivyo.
Unyama waliofanyiwa na Ajax kwenye michuano ya klabu bingwa kwenye hatua ya 16 bora ni kitu kingine kinachowapa maumivu matajiri hao kujishughulisha mapema ili kukwepana na wimbi kubwa la kukosa wachezaji wenye uwezo wa kukibeba kikosi hicho ili kupata matokeo.
Kuwawahi wengine kama PSG, Manchester United na Liverpool waliokuwa wanamnyemelea mlinzi huyo ni hatua kubwa sana klabu hiyo imepiga. Itakumbukwa wakati wa mechi yao dhidi ya Ajax mlinzi wao wa muda wote, Sergio Ramos hakuwepo kutokana na adhabu aliyokuwa anaitumikia hivyo kufanya safu yao ya ulinzi siku hiyo kupoteana kabisa. Ili kukamilisha mapinduzi hayo, Madrid hawana budi kusajili wachezaji kama:
Christian Ericksen, nyota huyo na kiungo wa Spurs amekuwa kiungo muhimu sana kwenye kikosi chao kwa kufanya majukumu muhimu akiwa kama kiungo. Endapo Madrid watamnasa itakuwa wamefanikiwa kwa kiwango fulani;
Mauro Icardi, nyota huyo wa Inter Milan mambo yake na utawala wa klabu hiyo bado hayajatulia na kuna uwezekano mkubwa akaondoka klabuni hapo ili awe huru zaidi hivyo akitua kikosini hapo watatisha sana.
Paul Pogba, tayari ameanza kuudhihirishia ulimwengu kwa nini United walitoa zile milioni kwa ajili ya usajili wake. Ni aina ya wachezaji wenye jicho la mbali kisoka na akiwa uwanjani. Ameweza kuipeleka United kule ambako wengi wakitamani kuiona klabu hiyo ikifika. Kwa fununu zinazoshika kasi kama akitua viwanja vya Bernabeu atakuwa msaada mkubwa.
Kylian Mbappe, naye yupo kwenye orodha ya majina ambayo klabu hiyo inayahitaji kikosini hapo lakini wanakutana na upinzani mkubwa kutoka kwa PSG wanaommiliki kwa sasa. Mbali na huyo bado hawakati tamaa kumfukuzia Eden Hazard kutoka Chelsea ili atue kikosini hapo.
Povel tz
Habar njema