Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania imesema kuwa haitamfuatilia tena Klyan Mbappe msimu ujao wa joto ikiwa hana nia ya kuondoka Paris Saint German (PSG). Mchezaji huyo ambae ni muhimu bado katika kikosi cha Galtier.

 

Madrid Kuhusu Mbappe

Miamba hao wa Hispania wamekuwa wakitamani sana kumleta supastaa huyo wa Ufaransa Bernabeu katika majira ya hivi majuzi ya uhamisho. Mbappe ambaye ana miaka 23, alitarajiwa kujiunga na Real msimu wa joto kwa mkataba wa hali ya juu, lakini bila kutarajia akatangaza kusalia PSG mwezi Mei.

Hilo liliwaacha viongozi wa Bernabeu wakiwa wamekata tamaa na mkuu wa Laliga Javier Tebas akatishia hatua za kisheria dhidi ya mabingwa hao wa Ufaransa kutokana na mpango huo “wa kashfa” ambao ulishambulia “uendelevu wa kiuchumi wa soka la Ulaya”

Kwahiyo Real Madrid wamesema kuwa hawataendeleza harakati zao za kumfukuzia Mbappe ili kuzingatia wachezaji wa kutua wanojua wanataka kucheza katika klabu hiyo ambayo kwasasa wananolewa na Carlo Ancelotti.

 

Madrid Kuhusu Mbappe

Real Madrid mpaka sasa ndio vinara wa Laliga kwa point 18 ambapo wameshinda mechi zao zote za ligi walizocheza huku wakiwa hawajapata hata sare huku wapinzani wao wakuu Barcelona wakiwa wamewapita alama mbili tuu.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa