Real Madrid wako tayari kumuuza, Eden Hazard msimu huu wa joto, kulingana na ripoti nyingi huko Uhispania. Madrid ilitumia pauni milioni 130 kumsajili Hazard kutoka Chelsea mnamo 2019 lakini ameshindwa kuonyesha makali yake.

Hazard, ambaye amekuwa nje kwa majeraha msimu huu, alianza katika kichapo cha 2-0 dhidi ya Chelsea Jumatano jioni ambayo iliiondoa Madrid katika Ligi ya Mabingwa.

 

madrid, Madrid Kumuweka Hazard Sokoni., Meridianbet

Mchezaji huyo alikasirisha mashabiki wengi wa Los Blancos baada ya kamera za runinga kumnasa akicheka na kufanya mzaha na mchezaji mwenzake wa zamani wa Chelsea, Kurt Zouma dakika chache baada ya filimbi ya mwisho.

Hazard tangu wakati huo ameomba msamaha kwa mwenendo wake lakini kulingana na Marca, uongozi wa Madrid umeamua kuwa wako tayari kusikiliza ofa kwa msimu huu wa joto.

Wakati huo huo, ABC inaripoti kwamba Los Blancos itakuwa tayari kumruhusu Hazard aondoke kwenye dirisha lijalo la uhamisho ikiwa watapata dau la Euro milioni 50 (Pauni milioni 43.4).


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

madrid, Madrid Kumuweka Hazard Sokoni., Meridianbet

SOMA ZAIDI

13 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa