Real Madrid wameripotiwa kukubali dau la €50m (£41.7m) kutoka kwa Newcastle United kwa ajili ya Eden Hazard, lakini taarifa zinasema winga huyo amekataa kuhamia St James’ Park.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 amekuwa akihusishwa na kuondoka Santiago Bernabeu, kutokana na kuwa kwenye fomu mbaya huko Uhispania, ambayo imemfanya kuwa chini ya kiwango akipitwa na Vinicius Junior, Rodrygo na Marco Asensio.
Los Blancos wanaaminika kuwa tayari kuruhusu wachezaji sita wa kikosi cha kwanza kuondoka klabuni hapo mwezi Januari na Hazard ni mmoja wa wachezaji ambao wako tayari kujadiliana kuhusu ofa zao.
Kwa mujibu wa El Nacional, Newcastle wamewasilisha ombi la awali la €40m (£33.3m) na kuongeza €10m (£8.3m) katika nyongeza, ambayo imekubaliwa na rais wa Real Madrid Florentino Perez.
Hata hivyo, Hazard hana nia ya kuihama klabu hiyo katika dirisha la majira ya baridi kali au kujiunga na Newcastle, na yuko tayari kumalizia sehemu ya mkataba wake ambao unadumu hadi Juni 2024.
Ripoti hiyo inaongeza kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji angefikiria tu kuondoka iwapo atarejea Chelsea, ambako alikaa miaka saba kati ya 2012 na 2019.
Hazard ameichezea Real Madrid jumla ya mechi 59 katika michuano yote, akifunga mara tano pekee na kusajili pasi 10.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.
CHEZA HAPA