Madrid Walifanya Kosa Kwa Ronaldo

Julai 2018, ulimwengu ulishuhudia mchezaji bora duniani akiondoka Real Madrid na kujiunga Juventus. Kwa mujibu wa kocha wa Shakhtar Donetsk – Luis Castro, hili ni kosa kubwa kwa Los Blancos.

Cristiano Ronaldo alikuwa ndio muhimili mkuu kwa Madrid na aliwasaidia kubeba taji la UEFA misimu mitatu mfululizo kabla ya kutimka klabuni hapo na kuhamia Juventus.

Kuelekea mchezo dhidi ya Real Madrid, Castro amezungumzia suala hilo na kusema “Unapokuwa na mchezaji kama Ronaldo kwenye timu yako, hupaswi kabisa kuruhusu aondoke.

“Tunamuongelea mchezaji wa aina yake, mchezaji bora duniani ni mashine kubwa. Sitaki kumfananisha lakini kwangu Ronaldo ni mchezaji bora duniani. Anahistoria nyuma yake ambayo ni mfano wa kuigwa.

Cristiano Ronaldo baada ya kutwaa taji la UEFA 2018 alipokuwa na Real Madrid

“Aliondoka akiwa na miaka 11 na kujiunga Lisbon ili akawe mcheza mpira, aliiacha familia yake. Ronaldo ni mchezaji aliyejipandisha mwenyewe akiwa na uelewa wa aina yake.

“Kwangu mimi, Ronaldo ni mfano kwa watoto wetu. Watu wanamsema sana ‘je akifanya hivi, kwanini asitumie pesa nyingi kwenye mambo mengine?

“Majibu yake anayotoaga uwanjani kila mara akiwa anatambua alipotokea. Siku watakayotengeneza filamu ya Cristiano Ronaldo na watu wakaona alipotokea, namna alivyokuwa mchezaji wa soka. Watu watampatia thamani yake kubwa anayostahili.”

Ronaldo ameshatwaa mataji 5 ya ballon d’Or na mpaka sasa ameshaifungia Juventus magoli 69 katika michuano yote yangu alipojiunga nao.


Ondoka na Mkwanja Kwenye Tsh. 160,000,000

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu.

Soma Zaidi

32 Komentara

    Ronald ni mchezaji aliyejipandisha nyota ya umaalufu mwenyewe kwenye soka kutokana na kiwango chake cha kucheza

    Jibu

    Madrid kweli walifanya makosa makubwa sana kumuachia ronaldo saiz Madrid wangekuwa mbali sana

    Jibu

    madrid watamkumbuka sana ronaldo yaani hii inaitwa kuchezea shilingi katika tundu la choo

    Jibu

    Hata mie nilishangaa sana maamuzi yao haikuwa poa kumtoa Ronaldo#Meridianbettz

    Jibu

    Ronaldo na atakumbukwa sana madrid

    Jibu

    Perez alichangaia san kundoka kwa cr 7

    Jibu

    Ronaldo atakumbuka sana madrid

    Jibu

    Ni pengo kubwa kwao

    Jibu

    Nikweli Ronaldo ndio alio inyanyua Madrid kwamakombe yakila dizaini ila kwenye krabu kila mtu anaona anauwamuzi wake wakufanya natazidi kukumbukwa siku zote Madrid Ronaldo kwakazi yake aliyokuwa anafanya

    Jibu

    Haikupangwa awe Madrid

    Jibu

    Ndo bas tena imepita hyo

    Jibu

    Duh watamkumbuka

    Jibu

    Bonge la pengo

    Jibu

    Kuna wachezaji wengi kama Ronaldo nyuma ya panzia waitaji kuinuliwa ili waje waishangaze dunia hinakua si kitu kizuri kutazama sehemu moja kumtengeneza mtu kama mbadala wa Ronaldo hitaleta manufaa makubwa sana

    Jibu

    Kosa hil

    Jibu

    makosa makubwa sana kumuachia ronaldo

    Jibu

    Duuh majanga hayo ni lazima akumbukwe kwa kile alichokifanya

    Jibu

    Cr anajua kaz yake

    Jibu

    Nic upadte

    Jibu

    Ni kwl ndo maana mzimu wake unawatafuta mpka leo pale Madrid

    Jibu

    Ronaldo Yuko vizuri Sana

    Jibu

    Madrid wanamkumbuka Ronaldo

    Jibu

    Mchezaji bola

    Jibu

    sana

    Jibu

    Ronaldo anajua kiwajigika

    Jibu

    kila kitu kina mwanzo wake na mwsh wk

    Jibu

    Cr7 atakumbukwa sana real madrid

    Jibu

    Ronaldo yupo vinzur

    Jibu

    Nikweli Ronaldo ndio alio inyanyua Madrid kwamakombe yakila dizaini ila kwenye krabu kila mtu anaona anauwamuzi wake wakufanya natazidi kukumbukwa siku zote Madrid Ronaldo kwakazi yake aliyokuwa anafanya

    Jibu

    Nature ya mchezaji mwenyewe CR7 huwa hakai timu moja muda mrefu ndio sifa kubwa nyingine inayoongeza ubora wake kulinganisha na timu nyingine

    Jibu

    Sana

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

Acha ujumbe