Beki na nahodha wa klabu ya Manchester United Harry Maguire inaelezwa anahitajika na klabu ya Aston Villa chini ya mwalimu Unai Emery.
Klabu ya Manchester United inaelezwa ipo tayari kumuuza beki huyo ghali iliyomnunua kutoka klabu ya Leicester City mwaka 2017. Klabu hiyo imekua ikisubiri ofa kutoka klabu yeyote ambayo itaonesha nia ya kumuhitaji beki huyo.Beki Harry Maguire amekua na misimu mibaya ndani ya klabu ya Manchester United huku akiwa moja ya wachezaji waliocheza chini ya kiwango kwa misimu takribani mitatu sasa, Klabu ya Aston Villa imeripotiwa kuhitahi huduma ya beki huyo wa kimataifa wa Uingereza.
Aston Vllla inahitaji huduma ya beki huyo ili kuimarisha safu yake ya ulinzi ambayo inaonekana eneo la beki wa katikati limekua na changamoto. Beki Tyrone Mings amekua ni beki asiyefanya vizuri ndani ya klabu hiyo hivo usajili wa Maguire utakua na tija kwa klabu hiyo.Harry Maguire kwasasa amekua hana nafasi kwenye kikosi cha Manchester United chini ya mwalimu Erik Ten Hag tangu kuanza kwa msimu huu. Hivo kuondoka ndani ya klabu hiyo na kujiunga na Aston Villa ni nafasi ya yeye kwenda kupata nafasi ya kucheza na vilevile kuweza kurudisha makali yake.