Maguire Kubaki Man United

Beki wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Harry Maguire huenda akasalia ndani ya klabu hiyo baada ya West Ham kutaka kuachana beki huyo.

Harry Maguire ambaye yeye mwenyewe inaelezwa hakua tayari kuondoka ndani ya timu hiyo, Lakini West Ham wenyewe wameamua kuachana na beki huyo kwasababu ambazo hazijawekwa wazi.maguireManchester United ilishakubali kiasi cha paundi milioni 30 ambacho kilitolewa na klabu ya West Ham kwajili kupata huduma ya beki huyo raia wa kimataifa wa Uingereza, Lakini mpaka sasa dili linaonekana limekufa.

Taarifa mbalimbali zinaeleza inawezekana klabu ya West Ham ikarudi tena kwa beki huyo, Lakini wakati huohuo kuna vyanzo vinaeleza kua klabu hiyo kutoka jijini London inaweza kusajili beki mwingine ndani ya 24 zijazo.maguireBeki Harry Maguire inafahamika hayupo kwenye mipango ya kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag, Lakini beki huyo anaamini anaweza kubaki kikosini hapo na kuendelea kupambania nafasi yake.

 

Acha ujumbe