Maguire Kukaa Nje Wiki Kadhaa

Beki wa klabu ya Manchester United Harry Maguire anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa kutokana na majeraha ambayo ameyapata katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Aston Villa.

Maguire alishindwa kumaliza mchezo dhidi ya Aston Villa na nafasi yake kuchukuliwa na De Ligt na taarifa ambayo ameithibitisha yeye mwenyewe kua atakua nje ya uwanja kutokana na majeraha ambayo yanamkabili, Hivbo beki huyo atakaa nje ya uwanja kwa muda wa wiki kadhaa kama ilivyoelezwa.maguireHili ni pengo wazi kwa klabu ya Manchester United kwani kwa siku za hivi karibuni beki huyo raia wa kimataifa wa Uingereza amekua mchezaji anayefanya vizuri ndani ya klabu ya Man United, Hivo klabu hiyo inakwenda kumpoteza moja ya wachezaji wake muhimu kwasasa klabuni.

Timu ya taifa ya Uingereza nayo ambayo imetaja kikosi cha timu hiyo kwenye michezo ya kimataifa ambayo inafuata wiki mbili mbele jina la beki Maguire limekosekana, Hiyo inatokana na majeraha ambayo ameyapata beki huyo katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Villa na hiyo na baada ya kutoka kufunga goli kwenye mchezo dhidi ya Fc Porto kwenye michuano ya Europa League na kuikoa Man United na kipigo.

Acha ujumbe