Mainoo Afurahia Ten Hag Kubaki

Kiungo wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Kobbie Mainoo ameonesha amefurahia kocha wa klabu hiyo Erik Ten kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo kama kocha mkuu.

Kobbie Mainoo amezungumza hayo akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa ya Uingereza ambayo ipo kwenye michuano ya Euro nchini Ujerumani“Nina shukrani sana kwa Erik ten Hag, siwezi kumshukuru vya kutosha.”mainoo“Ameshinda vikombe viwili tayari, tunatumaini kuna zaidi vitakuja.”

“Ni jambo zuri kuwa na amani hiyo ya akili, tunajua ni meneja gani tutakayemrudia katika msimu mpya.”

Kiungo huyo ameonesha kua hata akishukuru hawezi kutosheleza kwakua kocha huyo ndio amempa nafasi kutoka timu ya vijana mpaka kua kikosi cha kwanza cha timu hiyo, Lakini pia hakusita kuonesha furaha yake juu ya kubaki kwa kocha huyo.mainooKocha Erik Ten Hag ataendelea kua kocha mkuu wa klabu hiyo msimu ujao huku mazungumzo ya kuongezewa mkataba mpya yakiwa yanaendelea, Jambo limemfurahisha sana kiungo kinda Kobbie Mainoo mwenye umri wa miaka (19)kutokana na uaminifu ambao amempa.

Acha ujumbe