Mainoo Aitwa Uingereza Mara ya Kwanza

Kinda wa klabu ya Manchester United Kobbie Mainoo (18) amefanikiwa kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kwa mara ya kwanza mapema leo.

Mainoo ambaye ameongezwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza mapema leo ambapo atakua sehemu ya kikosi cha Uingereza kwenye michezo ya kirafiki ya timu ya taifa ya Uingereza dhidi ya Brazil na Hispania.mainooKiungo huyo kinda amekua kwenye ubora mkubwa ndani ya kikosi cha Manchester United akipata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza cha timu hiyo, Jambo ambalo limemshawishi kocha wa imu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate.

Msimu huu umekua wa bahati sana kwa kinda huyo kwani kabla ya kuitwa kwenye timu ya taifa ya Uingereza, Magwiji kadhaa wa soka nchini Uingereza walishinikiza kijana huyo aitwe wakidai anaonesha ubora mkubwa sana ndani ya Man United.mainooKobbie Mainoo anafanikiwa kujumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kinachojiandaa na mechi mbili za kirafiki, Huku ikonekana asilimia kubwa wakiunga mkono kitendo hicho cha mwalimu Gareth Southgate kutokana na ambacho amekionesha uwanjani kinda huyo msimu huu.

Acha ujumbe