Mainoo Amwagiwa Sifa na kocha Southgate

Kinda wa klabu ya Manchester United Kobbie Mainoo amemwagiwa sifa na kocha wa timu ya taifa ya Uingereza siku chache baada ya kuitwa kwenye kikosi cha timu hiyo.

Mainoo ambaye amefanikiwa kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kwa mara ya kwanza huku akiwa na umri mdogo zaidi kikosini, Amepokea sifa kutoka kwa kocha wake kuelekea mchezo wa leo dhidi ya timu ya taifa ya Brazil.MainooKocha Southgate akimuongelea kiungo huyo amesema “Tuna furaha kubwa na Mainoo ameingia kikosini kikamilifu, Amekua na kiwango bora mazoezini hivyo hatutasita kumuweka uwanjani”

Kauli ya kocha huyo ni wazi imetoa mwanga kua kinda huyo ataweza kupata nafasi ya kucheza katika mchezo wa kirafiki utaopigwa usiku wa leo dhidi ya mabingwa mara tano wa kombe la dunia timu ya taifa ya Brazil.

MainooKiungo Kobbie Mainoo amekua kwenye kiwnago bora sana ndani ya kikosi cha Manchester United tangu apewe nafasi kwenye timu ya wakubwa, Huku ikiwa ni sababu iliyochochea mpaka kuitwa kwenye timu ya taifa ya Uingereza akiwa kwenye umri mdogo kabisa wa miaka 18.

Acha ujumbe