Mainoo Kupewa Mkataba Mpya Man United

Klabu ya Manchester United ipo kwenye mazungumzo ya kumpa mkataba mpya kinda wake kiungo Kobbie Mainoo ambapo mpaka sasa mazungumzo yanaendelea baina ya pande zote mbili.

Manchester United inaelezwa inapanga kumpa mkataba Mainoo hadi mwaka 2030 mkataba wa muda mrefu na hii imekuja kutokana na kiwango ambacho anakionesha kijana huyo mwenye miaka 18 tu.mainooKatika mazungumzo ya mkataba mpya baina ya Man United na upande wa kiungo huyo ni kumuongezea kiwango cha mshahara mchezaji huyo, Huku akifungwa ndani ya klabu hiyo kwa miaka sita zaidi.

Klabu hiyo ina mpango wa kumfanya kiungo huyo kua kwenye mpango wa muda mrefu wa klabu hiyo, Kwani timu hiyo inataka kuandaa timu mpya ambayo itakua na vijana wenye ubora ili kuirudisha klabu hiyo kwenye ubora wake.mainooKiungo Kobbie Mainoo amekua akionesha ubora mkubwa sana ndani ya timu hiyo tangu apewe nafasi kwenye timu ya wakubwa akitokea kwenye akademi ya klabu hiyo, Jambo liliwavutia Man United kufikiria kumpa mkataba wa muda mrefu kinda huyo.

Acha ujumbe