Maisha ya Zlatan Baada ya Soka

Miongoni mwa wachezaji ambao wameweza kujijengea heshima kubwa sana katika soka ni Zlatan Ibrahimovic, kutokana na kuyaishi maisha yake halisi katika ubora, uwezo na hata kutumia mbinu zake zote kuzipa timu alizoweza kupata nafasi ya kuzitumikia katika maisha yake ya kisoka kwa kipindi chote.

Kwa wakati uliopo anakipiga na Serie A akiwa katika harakati za kukusanya mafao yake ndani ya ligi hiyo ili aweze kuzipata zitakazotosheleza haja zake. Lakini, kwa wakati uliopo akiwa tayari na umri mkubwa aneweza kuweka bayana juu lini hasa ataaga maisha hayo ya soka na kuishi maisha mengine kama wengine.

Imekuwa kawaida kwa wakongwe wa soka kuzihama ligi zenye ushindani mkubwa na kuelekea katika ligi ambazo hazina ushindani mkubwa ikiwa na lengo la kutengeneza hela kwa kipindi hicho, japo wengine hufanya hivyo ikiwa ni sehemu ya mapenzi yao na soka kwa kuona ugumu kuzihama klabu zao kwa wakati huo jambo ambalo umri pekee huwa kikwazo kwao kuhama.

Kwake Ibrahimovic ambaye amechezea klabu kubwa kama PSG, United, Barcelona msimu huu unaweza ukawa wa mwisho kwake baada ya kufaidi kila lililojema mbele yake na kuondoka na vikombe vingi sana kwenye maisha yake ya soka jambo ambalo anajivunia kabisa kuweza kulifikia ambapo wengi hutamani pia.

Alipoulizwa juu ya kitu gani angependelea kukifanya kwa wakati uliopo baada ya kuachana na soka, aliweza kuweka wazi kwamba anatamani sana kama angejiunga na wacheza filamu ili aweze kuucaa uhusika fulani kwa sababu kwa sasa akistaafu haangalii tena kujiunga na ligi yoyote ile ya soka.

Anatamani awe muigizaji ili aweze kuruka hapa na pale katika majengo marefu ili kutokana na nafasi hiyo aweze kutimiza lengo lake hilo ambalo alikuwa akitamani kulifanyia kazi kwa musa mrefu sana. Uhusika huo unamfaa kabisa kwa sababu umri wake bado unamruhusu kuyafanya hayo jambo ambalo halileti wasiwasi kwake.

Katika sehemu yake ya mafanikio ni kuweza kufikisha idadi ya magoli 500 katika historia yake ya maisha ya soka; na anapewa heshima yake kubwa kwa hatua hiyo ya pekee na ya kihistoria. Wengi sana wanatamani kupafikia hapo lakini ni wachache wanapata nafasi kupafikia; anaungana katika nafasi hiyo na wachezaji wengine kama Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ambao wamefikia kiwango hicho.

Ibrahimovic hataki mbegu yake ipotee anajitahidi kuisia vizuri ili izaliane zaidi na kuleta kila alichokiacha yeye mbele ya uso wa wengi ili kufanya historia na mazuri yake yasipotee. Anachojivunia kwa sasa ni kuwafanya watoto wake kuchagua upande wake wa soka ambao umeweza kumjengea mafanikio kwa kiasi kikubwa. Jambo ambalo analiona kabisa kwamba kile alichokifanya yeye kinakuja kwa awamu nyingine kwa wanawe hao Maximilian na Vincent.

Yatatimia? Tumpe muda!

3 Komentara

    Gud news

    Jibu

    Hongera sana kwake

    Jibu

    Habari nzuri hongera Sana ibramovic

    Jibu

Acha ujumbe