Ripoti zinasema kuwa Makamu wa Rais wa Galatasaray, Abdullah Kavukcu, amewasili nchini Italia kwa ajili ya kufanya mazungumzo kuhusu viungo kadhaa wa Serie A, akiwemo Teun Koopmeiners, Davide Frattesi na Youssouf Fofana.

Galatasaray wanatarajiwa kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na vigogo wa soka la Italia katika saa zijazo, baada ya Makamu wao wa Rais Abdullah Kavukcu kuwasili Italia kukutana na wawakilishi wa baadhi ya klabu za Serie A.
Habari hizi zilianza kuripotiwa na HT Spor nchini Uturuki kabla ya kuthibitishwa na vyanzo vya Italia, vikiwemo TMW.
Meridianbet inakwambia kuwa endelea kubashiri hapa kwani ODDS KUBWA na machaguo zaidi ya 1000 yapo hapa. Ingia kwenye akaunti yako na uanze safari yako ya ushindi sasa.
Kwa mujibu wa ripoti, Galatasaray wanavutiwa na kiungo wa Inter Davide Frattesi na Hakan Çalhanoğlu, Youssouf Fofana wa Milan pamoja na Teun Koopmeiners wa Juventus.
Inter wako tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya Frattesi na wameweka bei ya kuanzia euro milioni 35, huku kiungo huyo wa Italia akitafuta kuondoka Stadio Meazza mwezi Januari ili apate muda zaidi wa kucheza.


