Makosa ya Onyango Yalivyoigharimu Simba

Beki chaguo namba moja la Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck, mechi 11 zote ameanza kikosi cha kwanza ambazo Simba imecheza kwa msimu huu wa 2020/21.

Amefanya makosa matatu yaliyosababisha timu yake kufungwa mabao matano, kosa la kwanza ilikuwa Kwenye mchezo dhidi ya Ihefu, Uwanja wa Sokoine wakati Simba ikishinda mabao 2-1 katika harakati za kuokoa mpira alianua majaro, ngoma ilikutana na mchezaji wa Ihefu akamtungua Aishi Manula alikuwa ni Omary Mponda.

Kosa la pili ilikuwa wakati Simba ikifungwa bao 1-0 na Tanzania Prisons,  Uwanja wa Nelson Mandela, alimpoteza Aishi Manula kwenye harakati za kuokoa hatari mpira wa juu uliokutana na kichwa cha Salum Mbangula.

Kosa la tatu ilikuwa Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1  dhidi ya Yanga kwa kumchezea faulo Tuisila Kisinda iliyoleta penalti iliyofungwa na Michael Sarpong naye alifunga pia bao lake la kwanza kwenye dabi hiyo.

Kwa sasa Simba ina kibarua cha kuiwakilisha nchi kimataifa ambapo leo inatarajiwa kuanza safari kuelekea Nigeria ambapo kitapitia Ethiopia kabla ya kuunganisha mazima mpaka Abuja Nigeria siku ya Jumatano.

Kazi kubwa kwa Sven itakuwa ni kwenye safu ya ulinzi ambayo imekuwa ikiruhusu mabao kwa kuwa inakutana na timu yenye safu kali ya ushambuliaji jambo linalohitaji umakini zaidi.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

20 Komentara

    Natumain sven hata lifanyia kaZi yeye na beki nguli Deni ochien ONyango makosa Kama hayo hayatawez kujirudiah tena kila la kheri Simba. Wa kimataifa peperusheni benderi vzr watanzania tupo nyuma yenu huko

    Jibu

    Hawana. Jipya mikia a bahat yao tu sare wanashangilia

    Jibu

    Mapya haya

    Jibu

    Duuh majanga

    Jibu

    Majanga tuu

    Jibu

    Du atari

    Jibu

    wampe tu muda wamuangalie kama yatajirudia ama lah

    Jibu

    Ni kawaida katika mchezo kama timu ikipata matokeo mabaya basi lazima wa mtupie lawama mchezaji kwani alikuwa yuko pekeake uwanjani kupata matokeo uwanjani lazima mkubaliane nayo na kujifuza na kujirekebisha sio kukatishana tamaa katika klabu

    Jibu

    Mmmh makubwa

    Jibu

    Hatari

    Jibu

    Kutupiwa lawama kwa mchezaji ni changamoto kwa klabu ikifanya vibaya tu

    Jibu

    Duuh majanga haya

    Jibu

    Hizo ni changamoto za mpira

    Jibu

    Inabidi mjitaidi Aya makosa yasujirudie tena

    Jibu

    Hatari

    Jibu

    Ni kipindi kigumu sana kwa Onyango

    Jibu

    Dhuuu majanga

    Jibu

    Hizo ni changamoto zinazopatikana ktk mpira

    Jibu

    Duu majanga

    Jibu

    Tutafanyaje sasa tumempenda wenywe

    Jibu

Acha ujumbe