Malacia Aachwa Man United

Beki wa kushoto wa klabu ya Manchester United Tyrell Malacia ameachwa kwenye kikosi cha klabu hiyo ambacho kimeelekea nchini Marekani leo kujiandaa na msimu mpya.

Malacia ameachwa kwenye kikosi ambacho kimeelekea nchini Marekani kujiandaa na msimu mpya wa 2024/25 na hii ni kutokana na majeraha makubwa ambayo yamekua yakimuandama na kumueka nje kwa msimu mzima uliomaliza na mpaka sasa hajakaa sawa.malaciaKlabu ya Manchester United imethibitisha kua beki huyo hatakwenda nchini Marekani kama wenzake kwajili ya kujiandaa na msimu kwakua beki huyo bado hajaweza kurudi kwenye utimamu wake wa kiafya, Hivo ataendelea atabaki nchini Uingereza kuendelea na matibabu ili kurejesha utimamu wake.

Mbali na beki Malacia kuachwa kwenye kikosi cha Man United kuelekea nchini Marekani winga Jadon Sancho yeye amejumuishwa kwenye kikosi hicho licha ya kuhusishwa kutimka klabuni hapo, Lakini amejumuishwa kwenye kikosi cha klabu hiyo hii ikiendelea kuonesha inawezekana kwa kiwnago kikubwa akasalia kwenye kikosi hicho msimu ujao.

Acha ujumbe