Malacia Arejea Mazoezini United

Beki wa kushoto wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Uholanzi Tyrell Malacia amefanikiwa kuanza mazoezi ndani ya klabu hiyo baada ya kukaa nje msimu mzima.

Malacia ambaye alipata majeraha ya goti wakati wa kujiandaa na msimu mpya wa 2023/24 majeraha ambayo yalimfanya kukaa nje ya uwanja kw amsimu mzima uliopita, Lakini mapema leo ameonekana katika uwanja wa mazoezi wa Carrington akifanya mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya.malaciaTaarifa zinaeleza bado hajakaa sawa na kufanya mazoezi na wenzake ambapo mpaka sasa anafanya mazoezi ya peke yake huku akisimamiwa na timu ya madaktari ya klabu hiyo, Hii ni kuhakikisha anakua sawa kabisa kuelekea msimu unaofuata wa 2024/254.

Beki Malacia akiwa fiti kuelekea msimu ujao itakua faida kwa klabu ya Man United kwakua upande wa kushoto wa klabu hiyo utakua na watu wawili kwasasa, Kwani msimu uliomalizika alikua Luke Shaw peke yake na kipindi krefu cha msimu alikua nje ya uwanja hivo kupelekea beki Diogo Dalot kutumika kwenye eneo hilo.

 

Acha ujumbe