Ligi Kuu Nchini Afrika Kusini ijulikanayo kama DStv Premier League imefikia tamati June 5 Kwa Mamelodi Sundowns kutwaa taji la Ligi hiyo wakimaliza msimu na alama 67 na pengo la alama 13 kutoka Kwa Amazulu waliomaliza nafasi ya pili wakiwa na alama 54.

Mamelodi Sundowns

Limekuwa taji la 6 ndani ya misimu 10 ya mwisho Kwa “The Masandawana” huku likiwa la nne mfululizo. Tangu kuanza Kwa mfumo mpya wa Ligi Kuu Nchini humo 1996/97 Mamelodi Sundowns wamechukua taji hilo mara 11.

Kwa taarifa yako, Kwa sasa Mamelodi Sundowns ndo timu yenye mafanikio zaidi ndani ya soka la Afrika Kusini. Uwekezaji wa Patrici Motsepe umeendelea kulipa.

mamelodi sundowns, Mamelodi Sundowns Watwaa DStv Premiership, Meridianbet
Patrice Motsepe

Tangu Patrice Motsepe awekeze ndani ya “The Masandawana” baada ya mfumo wa mabadiliko mwaka 2004 Klabu hiyo imeshachukua mataji mengi zaidi ya awali na kuweka rekodi kadhaa.

️-Ligi Kuu SA (PSL) 🏆 X8
-Nedbank Cup 🏆 X3
-Telecom knockout X2
-MTN8 X1
-TOTALCAFCL X1
-CAF super cup X1

✍️Timu ya kwanza kutoka Afrika Kusini Kushiriki michuano ya FIFA Klabu Bingwa ya Dunia na kumaliza nafasi ya 6.

✍️Klabu Bora ya Mwaka Barani Afrika mara 1 ikiwa ni 2016

✍️Klabu Bora ya Mwaka Nchini Afrika Kusini mara moja, mwaka 2016.

✍️Timu Bora ya Msimu ya Ligi Kuu Afrika Kusini, PSL mara 2. 2013/14 na 2015/16


MAANA KAMILI YA USHINDI KATIKA KASINO ZA MERIDIANBETI NI PAMOJA NA MCHEZO WA PANDA PANDA.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Panda Panda na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Gomes, Gomes : Sitafanya Usajili wa Kutisha., Meridianbet

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa