Mamelodi Sundowns Mabingwa AFL

Klabu ya Mamelodi Sundowns kutoka Afrika ya Kusini imefanikiwa kutwaa ubingwa michuano ya African Football League baada ya kuifunga klabu ya Wydad Casablanca jioni ya leo katika mchezo wa fainali.

Mamelodi Sundowns imefanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kuifunga Wydad Casablanca kwa mabao mawili kwa bila, Ambapo jumla ya mabao yaliyofungwa katika fainali ni 3-2 kwani Wydad walishinda mchezo wa kwanza kwa mabao mawili kwa moja.mamelodi sundownsFainali ilikua yenye kuvutia lakini klabu ya Wydad walionekana kuanza mchezo huo wakienda na mpango wa kuzuia kutokana na kua na faida ya mabao mawili ambayo waliyapata katika fainali iliyopigwa jijini Casablanca wikiendi iliyopita.

Mshambuliaji Peter Shalulile ambaye alikua na majeraha na kurejea katika mchezo wa leo ndio alifanikiwa kuipatia Masandawana bao la uongozi katika kipindi cha kwanza na kufufua matumaini kwa klabu yake kutwaa ubingwa huo.mamelodi sundownsKipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Mamelodi Sundowns waliendelea walipoishia wakionekana kuhitaji bao lingine ili kujihakikishia ubingwa na walifanikiwa, Kwani dakika ya 53 Modiba aliweka bao la pili na kuipa uongozi wa bao mbili ambazo zilidumu mpaka mwisho wa mchezo na Masandawana kutawazwa kua mabingwa wakwanza wa AFL.

Acha ujumbe