Mamelodi Sundowns Waachana na Rulani Mokwena

Klabu ya Mamelodi Sundowns kutoka nchini Afrika ya Kusini wameamua kuachana rasmi na aliyekua kocha wa klabu hiyo Rulani Mokwena kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Klabu ya Mamelodi Sundowns imekua ikifanya vizuri sana nchini Afrika ya Kusini wakitawala ligi hiyo kw azaidi ya misimu mitano sasa, Lakini wameamua kuachana na kocha wao Rulani Mokwena ambaye anatajwa kama moja ya makocha bora sana barani Afrika kwasasa.mamelodi sundownsSababu za kocha huyo kutimka ndani ya klabu hiyo mabingwa wa ligi kuu nchini Afrika Kusini ni kutokua na maelewano mazuri baina yake na mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo anayefahamika kwa jina la Flemming Berg ikiwa ndio sababu kubwa ya kocha huyo kutimka klabuni hapo.

Mkurugenzi huyo wa michezo inaelezwa hakufurahishwa na muenendo wa klabu hiyo kwakua lengo lao kubwa zaidi ni kutwaa zaidi taji la ligi ya mabingwa Afrika, Lakini kocha huyo hakufanikiwa kutwaa tahi hilo jambo ambalo halijawafurahisha mabosi wa klabu hiyo.mamelodi sundownsKocha Rulani Mokwena amekua na mafanikio ndani ya klabu ya Mamelodi Sundwons katika miaka minne ambaye amedumu klabuni hapo akifanikiwa kutwaa matji saba ikiwemo mataji manne ya ligi kuu ya Afrika kusini, Lakini pia taji la African Football League ambalo lilianzishwa mwaka jana huku taji la ligi ya mabingwa Afrika ndio likimtia doa klabuni hapo mpaka anaondoka.

Acha ujumbe