Mabingwa wa ligi kuu ya Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns wametawala kwenye tuzo za ligi hiyo za mwaka huu kutokana na mchezo mzuri walioonesha kwenye michuano hiyo msimu huu.

Peter Shalulile ametangazwa Mchezaji Bora wa msimu wa Ligi kuu ya Africa kusini [DSTV Premiership]. Shalulile ameiwezesha Mamelodi kutetea taji Lao baada ya kufunga mabao 13 na Assist 6 katika mechi zote za Ligi alizoichezea Sundows.

Themba Zwane ametangazwa kiungo bora wa msimu baada ya kuwa na msimu mzuri ndani ya Sundows kwa kufunga mabao kumi na kuhusika kupika magoli matatu akiwa na Uzi wa Mamelodi ndani ya DSTV Premiership.

Denis Onyango Kipa wa Kimataifa Kutoka Uganda anayekipiga kwa Matajiri wa Pretoria Sundows ameshinda tuzo ya kipa bora wa Msimu baada ya nyavu zake kutokuguswa katika mechi 15 akiwa Dimbani.

Naye kocha Kijana anayekuja kwa kasi Benny McCarthy ametangazwa kocha bora wa Msimu baada ya kuongoza Amazulu kuwa na Msimu bora kabisa katika Historia ya Klabu yao kushika nafasi ya pili na kukata tiketi ya Kushiriki CAF Champions League Msimu ujao 2021-22.

McCarthy alichukua kijiti cha kuinoa Amazulu wakiwa nafasi ya 14 na kuwaongoza hadi nafasi ya pili nyuma ya Mabingwa Mamelodi Sundows hatua hii imempa nafasi ya kuwa kocha bora wa Msimu Kongole kwake kwa kazi nzuri aliyofanya ndani ya Amazulu Kutoka timu ya kupigania kushuka Daraja hadi kupigania ubingwa.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa