Ni muendelezo wa mafanikio katika klabu ya Man City kwa miaka 4 chini ya Pep Guardiola. Msimu wa EPL 2020/21 unaelekea ukingoni kibingwa zaidi!

City wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa EPL baada ya majirani zao – Manchester United kupoteza mchezo dhidi ya Leicester City.

United alikuwa Old Trafford akichuana na The Foxes ambapo mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa, The Red Devils walikuwa wameshapigwa 2-1. Kupoteza mchezo jana usiku, kumewapa ubingwa City ambao wapo kileleni kwa pointi 10 tofauti na United zikiwa zimesalia mechi 3 msimu kumalizika.

Man City, Man City Bingwa wa EPL 2020/21., Meridianbet
Sergio Aguero anaondoka City akiwa ametwaa makombe 4 ya EPL na klabu hiyo.

Kama ilivyo kwa Fulham ambao wameshuka daraja kwa tofauti ya pointi 1, Man City wanabeba ubingwa kwa tofauti ya pointi 1 endapo United atashinda na City atafungwa michezo yote ya EPL iliyosalia.

Hili ni taji la 4 la EPL kwa Man City wakiwa chini ya Pep Guardiola lakini ni taji lao la 5 ndani ya miaka 10. Haya ni mafanikio ambayo yanawafanya Man City kuwa na idadi sawa ya makombe ya EPL na Chelsea.

Licha ya kutwaa ubingwa wa EPL, Pep Guardiola amekiri EPL ni ngumu. Pep amenukuliwa akisema ” Huu umekuwa ni msimu na ubingwa wa EPL tofauti na mingine. Huu ulikuwa ni mgumu zaidi. Daima tutaukumbuka kwa namna tulivyoshinda. Ninajivunia kuwa meneja wa hapa na wachazaji hawa.

“[Wachezaji] niwakipekee. Kuvishinda vikwazo vyote tulivyopitia na kuonesha ubora wetu bila kusuasua, ni jambo kubwa. Kila siku wapo, wanapambania mafanikio, wanajaribu kuwa bora zaidi. Wamekuwa wavumilivu sana.

“Nimewahi kuwa Hispania, nimewahi kuwa Ujerumani na ninaweza kusema hii ndio ligi ngumu zaidi kwa hiyo inamaana kubwa kwa kila mmoja.” 

Kushinda kwa Leicester City dhidi ya Man United, kunatia doa imani ya Liverpool kuingia nafasi 4 za juu. Vita ya nafasi ya 4 bado ipo kwa Chelsea, Leicester City na West Ham United huku Liverpool wakiwa nafasi ya 5 na watasafiri kuwafata United alhamisi hii.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Man City, Man City Bingwa wa EPL 2020/21., Meridianbet

CHEZA HAPA

8 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa