Man City Kuvunja Benki Usajili Wa Grealish 2021/2022

Miezi Kadhaa iliyopita, Man City walihusishwa sana na kuhitaji saini ya Jack Grealish ambaye amekuwa nyota wa Aston Villa na kufanya poa sana kwa msimu huu klabuni hapo.

Grealish ana miaka 25 na kwa msimu huu uliokamilika ameonesha kiwango kikubwa sana akiwa na Aston Villa kiasi cha kuchukua mashiko ya klabu nyingi za England ikiwemo Manchester United na Man City yenyewe.

Msimu uliopita Grealish alihusishwa sana kujiunga na Man United lakini dili hilo halikufanikiwa kutokana na  ukosefu wa pesa za kutosha katika klabu hiyo yenye maskani yake pale Manchester!

man city na grealish

Aston Villa ina mkataba na Grealish mpaka 2025 na wameweka dau la pauni milioni 100 kwa mchezaji huyo kwa timu yoyote itakayohitaji huduma ya mchezaji huyo, huku City wakisema watavunja kabati kutaka huduma ya mchezaji huyo.

Kocha wa Man City, Pep Guardiola ni mnazi mkubwa sana wa Grealish na ametaja jina la Grealish na City wapo tayari kuvunja benki ili kunyakua saini ya mchezaji huyo!


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

Acha ujumbe