Man City wanaripotiwa kuwa wanakaribia kumnasa kiungo wa Gremio Diego Rosa.

Mchezaji huyo wa miaka 18 amekuwa akihusishwa sana na kikosi cha Pep Guardiola mwaka huu, lakini miamba hawa wa Uingereza hawakuweza kukamilisha makubaliano wakati wa dirisha la uhamisho wa majira ya joto.

KWA nujibu wa Manchester Evening News, Man City sasa wamekubali dili la kinda huyo, ambaye anaweza kuwagharimu pauni milioni 5.2 kama ada ya awali, ingawa dau linaweza kuongezeka hadi £ 23m.

Taarifa zinataja kwamba Rosa anatarajiwa kutolewa kwa mkopo baada ya kuwasili, na timu ya Ubelgiji Lommel SK – ikitajwa kama uwezekano wa kinda huyu kuwepo kwa mkopo.

Kijana huyo bado hajacheza kwenye kikosi chake cha kwanza cha Gremio lakini uwezo na kiwango chake katika timu ya vijana ya chini ya miaka 17 ya Brazil i8mekuwa ikivutia vilabu vikubwa.


 

FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Man City, Man City Karibu Kuinasa Saini ya Diego Rosa, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

20 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa