Man City Kuvaana na United Saini ya Declan Rice

Man City wanaripotiwa kuwa tayari kupambana na Man United kuipata saini ya Declan Rice wa West Ham United msimu wa joto wa 2022.

Licha ya vilabu vyote vya Manchester kuwa na nia na saini ya staa huyu kwenye dirisha lililopita la uhamisho, Rice alisalia London, na bei yake ya pauni milioni 80 ikiwafukuza wanunuzi.

Hata hivyo, mpambano wa kuwania saini ya mchezaji huyo wa Uingereza kati ya Man United na Man City unatarajiwa kuanza majira ya kiangazi, na ripoti ya hivi karibuni inataja kuwa Man United inaweka mambo yake vyema tayari kwa ajili ya kumwinda staa huyo.

Man City Kuvaana na United Saini ya Declan Rice

Vijana wa Ole Gunnar Solskjaer wanaweza kulazimika kuzuia masilahi ya Man City, lakini The Sun inadai kwamba Pep Guardiola anataka Rice kuchukua nafasi ya Fernandinho pale Dimbani Etihad.

Mbrazil aliongeza muda wake kuwepo Man City hadi 2022 mapema mwaka huu, lakini hatarajiwi kuendelea kuwepo zaidi ya mwisho wa msimu huu, licha ya kuwa anaweza kusalia klabuni hapo kwa majukumu mengine.

Rice amebakiza chini ya miaka mitatu kukamilisha mkataba wake na West Ham, na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anaendelea kuwa sehemu muhimu ya kikosi cha timu hiyo.


USHINDI KIGANJANI KWAKO!

Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.

Meridianbet Online Casino

 INGIA MCHEZONI HAPA

Acha ujumbe