Nyota wa Man City, Raheem Sterling ameripotiwa kuwa mmoja wa wachezaji ambao City wapo tayari kumtoa sadaka ili kukamilisha upatikanaji wa Harry Kane kutoka Spurs.
Baada ya Kane kubainisha kuwa yupo tayari kuachana na klabu yake mwishoni mwa msimu uliopita, City wamekuwa wakifanya juu chini kuangalia uwezekano wa kumleta Kane pale dimbani Etihad.
Ofa ya awali ya £100m ya Man City kwa nyota huyo inaripotiwa kuwa tayari imeshakataliwa, hivyo Man City kwa sasa wanajaribu kufikiria kuwahusisha wachezaji kama sehemu ya dili hilo.
Kwa mujibu wa ripoti za awali iliainisha kuwa Bernardo Silva, Riyad Mahrez na Gabriel Jesus kuwa kwenye mpango wa wachezaji wa kubadilishana kuongeza uzito kwenye dili hilo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa The Mirror, Raheem Sterling ameibuka kuwa kipaumbele kwenye chaguo la nani anaweza kutolewa sambamba na kiasi cha pesa ili kupata huduma ya Harry Kane.
Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!
Ernest
Mchango wa Sterling kwa City upo wapi??!!!!