Klabu ya Man City inamuwinda kiungo wa klabu ya Fc Barcelona ya nchini Hispania Frenkie de Jong raia wa kimataifa wa Uholanzi ili kuboresha kikosi chao kuelekea msimu ujao.

Klabu ya Man City baada ya kumkosa kiungo wa kimataiifa wa Uingereza Declan Rice ambaye amekubali kujiunga na klabu ya Arsenal, Hivo vijana wa Pep Guardiola wanamuona Frenkie de Jong kama mbadala sahihi wa Declan Rice.man cityMabingwa hao wa ligi kuu ya Uingereza walikua wanamuhitaji Rice lakini walizidiwa dau na Arsenal ambao wametoa paundi milioni 105 ambapo City wao walikua na dau la paundi milioni 90 kitita ambacho kilipigwa chini na klabu ya West Ham.

Man City wanaona kiasi cha paundi milioni 90 kinaweza kutosha kuishawishi klabu ya Barcelona kuwauzia klabu ya Barcelona, Kwani Barcelona wamekua wakipitia kipindi cha mpito cha kukosa hela na kiasi hicho cha pesa ni kikubwa sana.man cityKlabu ya Man City vilevile inatafuta mbadala pia wa nahodha wake Ilkay Gundogan ambaye amejiunga na klabu ya Barcelona, Hivo ni kama City wanataka kupishanisha viungo hao Gundogan Barca na Frenkie de Jong nae ajiunge na Mabingwa hao wa Uingereza.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa