Man City Yamvizia Kiungo West Ham

Klabu ya Man City ipo kwenye mkakati wa kumchukua kiungo wa klabu ya West Ham United raia wa kimataifa wa Brazil Lucas Paqueta ili ajiunge na mabingwa hao wa Uingereza.

Man City walipeleka dau la paundi milioni 70 kwa klabu ya West Ham kwa kutaka kumchukua kiungo huyo wa kimataifa wa Brazil, Lakini wagonga nyundo hao wa London walikataa na kupiga chini ofa hiyo.Man CityMabingwa hao wa soka nchini Uingereza na ulaya kwa ujumla wanapanga kuboresha ofa yao na kutuma tena kwa West Ham kwakua wana uhitaji mkubwa na kiungo huyo wa zamani wa klabu ya Olympique Lyon Lucas Paqueta.

Kiungo Paqueta amekua kwenye kiwango bora ndani ya klabu ya West Ham United na kua moja ya wachezaji tegemezi ndani ya klabu hiyo, Jambo ambalo limeivutia Man City kutaka huduma yake.Man CityWest Ham wameweka ugumu kwenye kiwango ambacho mabingwa hao wa Uingereza wamekiweka mezani, Huku wakihitaji zaidi ya paundi milioni 70 ambapo mpaka sasa West Ham inaonekana ni klabu iliyovunjwa zaidi kwenye ligi kuu ya Uingereza msimu huu.

Acha ujumbe