Man United Kuamua Kuhusu Lingard.

Kimsingi, kwa hali ilivyo kwa sasa, Man United ndio wataamua kama Lingard anaondoka sasa hivi au mwisho wa msimu.

Newcastle United wameweka mezani kila walichojipanga nacho ili kumsajili Lingard Januari hii. Kwa upande wa Jesse mwenyewe, hana mpango wa kubaki United baada ya mkataba wake kumalizika msimu huu. Hana tatizo na kwenda St. James’ Park kwa nusu ya msimu huu iliyosalia. Kikwazo ni United.

Inaripotiwa kuwa, Man United haijatoa jibu lolote kwa Newcastle mpaka sasa. Japokuwa, uongozi wa The Magpies unaendelea kuweka jitihada kukamilisha hili ndani ya siku chache zilizobaki kwenye dirisha hili la usajili.

Wanachokifanya United pengine kinaweza kuwagharimu zaidi mbeleni. Lingard amebakiza miezi michache kumaliza mkataba wake na timu hiyo. Endapo hatotolewa kwa mkopo au kuuzwa majira haya, United wajiandae kutoka patupu ifikapo Juni 30, 2022. Muda huo, Lingard atakua mchezaji huru na United haitohusika na hata thumni ya usajili wa mchezaji huyo.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe