Kule London bado hakujapoa, suala la usajili wa Harry Kane bado lipo chini kwa chini. Ripoti zinasema, Man United wanauwezekano wa kuwapiku Man City na Chelsea.

Kocha wa Man City, Pep Guardiola, alisema wazi kuwa kutokana na gharama wanazotajiwa kwenye mchakato wa kusajili washambuliaji, kuna uwezekano mkubwa hatosajili mchezaji kwenye nafasi hiyo majira haya ya usajili.

Chelsea bado wanajitafuta katika kufanya maamuzi, watoe kitita kirefu kwa Kane au Haaland. Lakini pia suala la mahusiano kati ya Chelsea na Spurs (mahasimu wa jiji la London) ni jambo lingine gumu kulikwepa.

Kwa Man United mambo ni tofauti kidogo, wameshatoa £73M kwa usajili wa Jadon Sancho pekee na hii inaonesha ni kiasi gani United wanajambo lao msimu ujao. Inasemakana yanayoendelea chini ya kapeti, yanawapa nguvu United kuliko City na The Blues.

Inasemekana Spurs wapotayari kumuachia Kane kwenda United kama timu hiyo itatoa £100M na wachezaji wawili wa kikosi cha kwanza. Japokuwa haijawekwa wazi ni wachezaji gani wanaohusishwa na mchakato huu, lakini Man United wanauwezo wa kuwatoa baadhi ya wachezaji kama kweli wanalengo la kumsajili Kane msimu huu.

Swali ni Je, ni kweli Harry Kane (miaka 27) anathamani hii ambayo Spurs wanamuwekea? Ni uhalisia kwa United kufanya usajili wa gharama hii? Wachezaji watakaotolewa na United ni wapi?


KUSANYA PESA HAPA!

IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!Meridianbet

INGIA MCHEZONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa