Man United Mazungumzoni na Fernandes

Manchester United wanatajwa kuwa katika mazungumzo na Bruno Fernandes juu ya mkataba mpya huko Old Trafford.

Mchezaji huyo wa miaka 26 amekuwa mchezaji muhimu kwa Mashetani Wekundu tangu alipowasili kutoka Sporting Lisbon Januari 2020, akifunga mabao 40 na kusajili asisti 25 katika mechi 80 za mashindano yote.

MSimu uliopita, mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno alifunga magoli 28 na kusajili asisti 17 kwenye mechi 58 za klabu, akiwa bado amebakiza miaka minne ya mkataba wake huko Old Trafford.
Bruno Fernandes Man United

Hata hivyo, kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Italia Fabrizio Romano, mabingwa hao wa Uingereza wa mara 20 kwa sasa wanajadiliana na Fernandes na wakala wake juu ya mkataba mpya.

Romano anadai kuwa Mreno huyo anatarajiwa kupewa mshahara wa juu zaidi kila wiki ili kuonyesha umuhimu wake chini ya Ole Gunnar Solskjaer.


JIUNGE NA FAMILIA YA MABINGWA!

Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!

Italia, Italia Bingwa Euro 2020., Meridianbet

JIUNGE SASA!

Acha ujumbe