Man United: Hatujapokea Ofa Yotote kwa Pogba

Manchester United wanatajwa kuwa wapo tayari kumuacha Paul Pogba aondoke, lakini bado hawajapokea ofa ya dili lolote kuelekea dirisha la usajiri la mwezi Januari.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amebakiza zaidi ya miezi sita katika kandarasi yake pale Old Trafford na hakuna dalili zozote za kujadili mkataba mpya.

Kwa mujibu wa Manchester Evening News, mkufunzi wa muda Ralf Rangnick yuko tayari kumruhusu Pogba kuondoka klabuni hapo dirisha la Januari lakini, Mashetani Wekundu bado hawajapokea ofa kubwa kwa Mfaransa huyo.

Ripoti hiyo inaongeza kuwa United hawakuweza kusajili kiungo mpya wa kati msimu uliopita wa joto kwani waliamua kuupa kipaumbele usajili wa Jadon Sancho, Raphael Varane na Cristiano Ronaldo, wakitumia zaidi ya £100m katika mchakato huo.

United walikuwa wanavutiwa na Declan Rice wa West Ham United na Eduardo Camavinga wa Rennes, ambaye sasa yuko Real Madrid, ingawa dili la mchezaji yeyote kati yao lilishindikana.

Huku Jesse Lingard na Juan Mata pia wakimaliza kandarasi msimu ujao wa joto, Rangnick sasa anatumai kuajiri kiungo mpya katika Mwaka Mpya.

Pogba, ambaye amewahi kuwaniwa na Real Madrid na Paris Saint-Germain, hajacheza mechi United tangu walipopokea kipigo cha 5-0 dhidi ya Liverpool mwezi Oktoba kutokana na jeraha la misuli ya paja.


KUWA BINGWA MSIMU HUU WA SIKUKUU NA OCEAN CALL

Nani hapendi kuwa bingwa na kujishindia mkwanja wa kusahato kuelekea katika sikukuu wiki hii. Mchezo wa Ocean Call kutoka kasino maridhawa za meridianbettz unakupa kila sababu ya kuifanya siku kuu yako kuwa ya kuvutia zaidi.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.