Man United Kutuma Skauti kwa Michael Olise!

Manchester United inaweza kutuma skauti kumtazama Michael Olise akiichezea Crystal Palace katika mechi ya Jumapili ya robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya Everton. Kwa mujibu wa taarifa.
Man United Kutuma Skauti kwa Michael Olise?
Michael Olise

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 amekuwa katika kiwango bora akiwa na The Eagles kwenye kampeni hii ya 2021-22, akifunga mara nne na asisti nane kwenye mechi 26 za mashindano yote.

Olise ana mkataba Selhurst Park hadi Juni 2026, lakini inaaminika kuwa uchezaji wake msimu huu umevutia vilabu vingi.

Kwa mujibu wa gazeti la Manchester Evening News, Man United wanaweza kumtazama chipukizi huyo wakati Palace wakimenyana na Everton kwenye Kombe la FA Jumapili.

Ripoti hiyo inadai kwamba Palace sasa wanamthamini mshambuliaji huyo kwa takribani £24m na watakuwa tayari kupokea ofa kubwa wakati wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi.

Olise alifunga mara saba na asisti14 katika mechi 73 alizochezea Reading kabla ya kuhamia Palace msimu wa joto wa 2021.


SHAOLIN FORTUNES 100 ONJA LADHA YA USHINDI

Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.

liverpool, Liverpool Kila Mtu Ashinde Mechi Zake., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe