Kuelekea kwenye dirisha kubwa la usajili, Jadon Sancho haonekani kama usajili wa muhimu sana kwenye kikosi cha Man United.
United walitumia miezi 2 kuisaka saini ya Sancho msimu uliopita bila mafanikio baada ya Borussia Dortmund kuhitaji pesa ndefu ambayo United hawakuwa tayari kuitoa. Maisha yaliendelea baada ya usajili kukwama na msimu huu mambo yamekuwa tofauti.
Licha ya Chelsea, Liverpool na Manchester United kuhusishwa na Sancho, United hawaonekani kama wanaulazima sana wa kumsajili winga huyo msimu huu.
Mason Greenwood amekuwa kwenye kiwango kizuri msimu huu akicheza kama winga wa kulia na maendeleo yake, yanamfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wa muhimu zaidi kwenye kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer. Sambamba na Greenwood, suala la Cavani kuongeza mkataba wa kuendelea kubaki Old Trafford, linaendelea kuwapa nafasi Martial, Rashford na Greenwood kuendelea kupambania nafasi za mawinga.

Ubora wa Rashford na Greenwood sambamba na aina ya uchezaji wao, unaendana sana na ule wa Jadon Sancho. Hii inawaweka Man United kwenye nafasi ya kuzitazama nafasi zingine zinazohitaji maboresho kuelekea msimu ujao kuliko kumsajili Sancho.
Ukiachana na waingereza hao, Paul Pogba ameendelea kuwa kwenye ubora wake akicheza upande wa kushoto huku Bruno Fernandez akitawala kwenye nafasi ya kiungo mshambuliaji nyuma ya Edinson Cavani. Hawa ni baadhi ya wachezaji ambao hawaonekani kukosa namba kwenye kikosi cha United kwa siku za usoni.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
Kama hela hamna mwacheni sancho
Asante kwa makala
Hayo ni maneno ya mkosaji
Kiwangi bado
United waangalie mambo mengine
Habar njema
Si mseme mmeishiwa
Watuachie Sancho wetu
Hipo sahii
Pesa nying uwez kawaida