Pengine Man United wamepuuzia waliyokumbana nayo kwenye usajili wa Jadon Sancho. Juhudu za misimu 4, hazikufua dafu kwa BVB. Kwa Camavinga, mjiangalie.
United walianza mchakato wa kuisaka saini ya Sancho toka 2018 na hawakufanikiwa. 2020 walijikuta wakicheza mchezo wa kutega mwishoni mwa msimu wakiamini Dortmund wangeshusha dau lakini waliambulia patupu.
Labda waliiona joto ya jiwe, 2021 mambo yamekuwa tofauti. Walianza mapema harakati za kumsajili Sancho na wamefanikiwa kumpata kwa dau dogo (£73M) ikilinganishwa na 2020 (£108M), hii ni kutokana na mkataba wake na BVB kubakiza mwaka mmoja tu.
Kwa Camavinga, Man United wajiangalie. Ni dhahiri wanahitaji kiungo mwingine wa kuimarisha nafasi hiyo na kimsingi, Camavinga ni kijana mdogo mwenye uwezo wa kulitawala dimba katikati.
Kinda huyu amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake na Rennes, licha ya kuwa klabu hiyo inaukata wa pesa – dau la £25M ni kiasi kidogo sana kwa United kutoa ili kumsajili Camavinga ambaye anaonekana kabisa hana mpango wa kuongeza mkataba Rennes.
Wanachokifanya United ni kuonesha dhahiri kuwa wanamtaka Camavinga lakini hawana haraka nae. Hapa ndipo wanapochanganya mambo na kucheza mchezo wa pata potea.
PSG, Real Madrid, Barcelona pengine na Man City na Chelsea wote wanamtolea macho Camavinga na wanaangalia kinachoendelea kati ya United na Rennes. Endapo United watapuuzia kumsajili kwenye dirisha hili na kiungo huyu hatosaini mkataba mpya – Man United wananafasi kubwa ya kumkosa kama ataingia kwenye kundi la wachezaji huru ifikapo Januari 1,2022.
Kwa Man United, kama kweli wanania na Camavinga ni wamsajili sasa hivi kwa dau dogo au wasubiri kucheza mchezo wa patapotea atakapokuwa mchezaji huru.
Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!
dorophina
Man u wafanye kweli wambembe kijana camavinga