Klabu ya Manchester United inafikiria kutoa ofa ya £50million kwa Leed kwaajili ya kufadhili usajili wa kiungo wa England, Kalvin Phillips katika majira ya kiangazi.

 

united, Man United Wanamtaka Phillips Old Traford., Meridianbet

United wanafikiria kuboresha eneo lao lao la kiungo katika majira ya kiangaza hasa baada ya tetesi za kuondoka kwa Nemanja Matic, Paul Poga na Jesse Lingard katika majira ya kiangazi.

Phillips, 26 amekuwa mchezaji bora katika ligi ya EPL tangu Leeds ilipopanda daraja, na kufanikiwa kuorodheshwa katika timu ya taifa ya England iliyotinga katika fainali ya Euro 2020.

Phillips bado anamkataba kuendelea kusalia Elland Road mpaka mwaka 2024 akiwa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi katika kikosi cha Leeds, huku akiwa hajaongeza mkataba mpaka sasa.


BURUDIKA NA KASINO BOMBA ZA MTANDAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa