Dembele ameripotiwa kuwa hahitaji tena kuondoka Barcelona katika dirisha lijalo la uhamisho.
Nyota huyu amekuwa sehemu muhimu sana ya kikosi cha Barca kwa msimu huu 2020-21, akiwa amecheza jumla ya mechi 36 na kufunga magoli 10 na asisti nne.
Licha ya mkataba wa staa huyu kuwa mbioni kuisha mwezi Juni, Manchester United wamekuwa wakihusishwa zaidi na kuingia sokoni majira ya kiangazi.
Man United ilikuwa wamsajili kwa mkopo staa huyu katika dirisha la uhamisho la kiangazi kilichopita, lakini Barcelona wakachomoa waya mwishoni katika dili hilo.
Dembele anatambua kuwa United wamemuweka kwenye rada zao, na wanafanya mipango ya kupata huduma yake, lakini Mundo Deportivo wanasema yeye bado hajataka kuachana na kikosi cha Ronald Koeman.
Mashetani wekundu wanahitaji kupata mbadala wa huduma yake sokoni, hasa kwa kuzingatia Barcelona wanataka kulishikilia suala la mkataba mpya wa Dembele kama kipaumbele kwa sasa.
Dembele ambaye amecheza jumla ya mechi 110 na Barcelona, na kufunga jumla ya magoli 29 na kutoa asisti 20 kwenye jumla ya mechi 110, pia alivitua baadhi ya vilabu toka Serie A wakiwemo Juventus.
INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.
Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.
CHEZA HAPA
Adelta
Manchester united watafute mbadala mwingine badala ya Dembele
warda
Kwa kweli wafanye hivyo