Wachezaji wa Man United wang`ara huku timu ya taifa ya Ureno ikishinda magoli manne kwa bila dhidi ya jamhuri ya Czech usiku wa jana katika dimba la Fortuna Arena.

Wachezaji wa klabu ya Man United wanaoitumikia timu ya taifa ya Ureno walikua kwenye ubora mkubwa katika mchezo huo baada ya kusaidia kupatikana magoli yote manne yaliyopatikana katika mchezo huo.

man unitedDiogo Dalot aliekua kwenye kiwango bora kabisa usiku wa jana alifanikiwa kufunga magoli mawili katika mchezo huo  kiungo Bruno Fernandes akifanikiwa kufunga bao na kuipiga pasi moja ya bao katika mchezo huo huku staa na nahodha wa timu hiyo akipiga pasi moja ya bao kwenda Diogo Jota alifunga katika mchezo huo na kuonesha namna gani wachezaji wa Man United wamechangia kwa kiasi kikubwa ushindi wa timu hiyo.

Mchezo huo umefanya timu ya taifa ya Ureno kukwea kileleni mwa kundi la 2 baada ya kufikisha alama 10 mbele ya timu ya taifa ya Hispania yenye alama 8.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa