"Man Utd Iachane na Pochettino na Ten Hag" Ally McCoist

Ally McCoist anaamini Man Utd inapaswa kuanza mchakato wa kuwafuatilia Zinedine Zidane au Diego Simeone dhidi ya Mauricio Pochettino au Erik ten Hag kwenye majira ya kiangazi ambapo klabu hiyo itahitaji mkufunzi mpya.

Klabu ya mashetani wekundu inapanga kumteua kocha atakaye chukua majukumu ya kuinoa klabu hiyo baada ya kocha wa muda Ralf Rangnick ambaye alichukua mikoba mwezi December ya kuinoa klabu hiyo baada ya Ole Gunnar kufungashiwa virago kwenye klabu hiyo.

Man Utd

Zidane na Simeone hawakuwepo kwenye majina ambayo yaliopendekezwa kwenye klabu Man Utd kama miongoni wa makocha ambao wanawaniwa na klabu hiyo.

“Najua watu wanazidi kusema kuwa Zidane hazungumzi kingereza na haitaji kuishi hapa, lakini yeye na Simeone ni majina pekee ambayo ambayo yanaweza kubeba mikoba mikubwa.” Alisema McCoist

“Pochettino, sina hakika. Alifanya kazi kubwa akiwa Tottenham na amefanya kazi kubwa akiwa PSG, Ten Hag, kuwa mkweli, simfahamu vya kutosha.

“Lakini jambo moja, kwa hakika inabidi waweke mambo sawa ili mambo yaende. Kuwa na idadi kubwa ya makocha ambao watainoa timu hiyo tangu Sir Alex Ferguson aondoke lakini bado sio jibu.”


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

 

 

Acha ujumbe