Klabu ya Man Utd imetangaza udhamini mpya na kampuni ya technology ya DMX kutoka nchini Marekani kama mdhamini mpya wa msimu wa 2022/23 ambaye logo yake itawekwa mkononi baada ya kampuni Kohler kumaliza muda wake.
DMX inakwenda kuchukua nafasi ya kampuni ya Kohler ambayo inajihusisha na utengenezaji wa vyombo vya jikoni na chooni, Kohler ni kampuni ya kwanza kuidhamini klabu ya Man Utd kwa upande wa mkononi tangu mwaka 2018.
Mdhamini mkuu wa klabu ya Manchester anabaki kuwa kampuni ya technology ya TeamViewer baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano ya udhamini kwenye majira ya kiangazi mwaka jana.
Mpaka sasa klabu ya Man Utd haijatangaza jersey zake mpya, lakini tayari zimeshavuja aina ya jersey watakazo tumia kwa misimu wa 2022/23, huku muundo wake ukifanana na jersey walizotumia mwaka 1990. huku wakati muundo wa kora na marembo yake ikiwa sawa na jersey iliyotumika kati ya mwaka 1998 na 2000.