Hamasa ya timu kushinda mechi au mataji mbalimbali huchangiwa kwa kiwango fulani na uwepo wa nahodha mzuri anayeweza kuihamasisha timu yake iweze kupambana na hata kutafuta matokeo pale wanapokuwa wameelemewa. Kwa lugha nyingine nahodha ni kovha wa timu ikiwa dimbani.
Mbali na uwezo wa kuhamasisha pia hupaswa kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kutafuta ushindi au hata 2akati anawasiliana na waamuzi hutakiwa kuondoa jazba kabisa na kuwa wa tofauto na msikivu. Baadhi ya manahodha bora kuwahi kushuka EPL na wakajenga historia kubwa ni hawa wafuatao;
Roy Keane, Manchester United; ni klabu yenye mafanikio makubwa sana katika historia ya ligi ya Uingereza ambayo waliijenga kuanzia miaka ya 1990 hadi katikati ya 2000. Ndani ya kipindi hicho waliweza kiongozwa na manahodha wenye ushawishi mkubwa sana akiwemo Keane. Aliichukua nafasi hiyo baada ya Cantona kustaafu kutokana na majeraha ambayo halikuwa yakimsumbua mara kwa mara akaamua kustaafu. Ameweza kushinda mataji saba.
Steven Gerrard, Liverpool; miongoni mwa historia mbovu aliyo nayo ni kukosa kabisa kushinda kombe la ligi akiwa kama kiongozi wa timu hiyo. Mbali na uwezo wake wa kuongea na timu yake lakini hajawahi kufanikiwa kabisa kunyanyua hilo kombe. Mbali na hapo aliwahi kujishindia kombe la FA mbele ya West ham. Majeraha ni dhahama nyingine akiwa kama mchezaji aliweza kukutana nayo.
John Terry, Chelsea; Mourinho ndiye alikuwa mtu wa kwanza kutambua nafasi ya Terry mwaka 2004/05 hilo ni kutokana na nidhamu aliyokuwa anaionesha ndani ya klabu hiyo. Aliweza kuiongoza klabu yake kuweza kushinda mataji akiwa kama nahonda na mlinzi huku akichangia sana kuzuia timu yake ipate matokeo bila kufungwa. Amewapa Chelsea mataji matano ya ligi matatu ya FA, klabu bingwa hata Europa.
Mbali na nao kuna majina mengine ambayo yamefanya vizuri pia kwa kuandika rekodi kubwa na ya pekee wakiwemo; Tony Adams, Arsenal aliyepewa cheo hicho na George Graham mwaka 1988, na Vincent Kompany, Manchester City ambaye ameitumikia klabu hiyo kwa moyo mmoja na kuipambania hadi kustaafu kwake kwa mafanikio makubwa sana na ya pekee. FA ndiyo kikombe cha awali kabisa kuweza kushinda katika uongozi wake ndipo akafuata mataji mengine. Kwa sasa amestaafu kuichezea klabu hiyo na anaanza majukumu mengine kama kocha mchezaji ndani ya klabu ya Anderchelet.
Furahav
Ni kwel.
Fatina mfingi
asnteh kwa taaifa meridinabet
Zeiyana
Asante kwa taarifa