Mchezo wa kibabe kati ya vilabu bora kwasasa nchini Uingereza kati ya klabu ya Manchester City dhidi ya Arsenal umemalizika kwa sare ya magoli mawili kwa mawili mchezo uliopigwa katika dimba la Etihad.
Manchester City walifanikiwa kupata goli la mapema kupitia kwa mshambuliaji Erling Haaland dakika 9 ya mchezo kabla ya beki Ricardo Calafiori dakika 22, Huku City wakionekana kutawala mchezo kwa kiwango kikubwa na Arsenal wao wakifanya mashambuli ya kushtukiza ambayo baada yalionekana kuwalipa.Kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika Arsenal walipata goli la pili kwa mpira wa kona uliochongwa vizuri na Bukayo Saka na beki Gabriel Magalhaes kuuweka wavuni dakika ya 45+1 kipindi, Huku dakika mbili mbele kwa maana ya 45+3 winga Leandro Trossard akionyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje ya uwanja na kipindi cha kwanza kumalizika kwa Arsenal kua mbele.
Kipindi cha pili kilionekana kua na taswira ya tofauti ambapo Arsenal walionekana kua nyuma zaidi kwani walikua pungufu ya mchezaji mmoja, Lakini pamoja na hivo walizuia kwa umakini mkubwa huku Golikipa David Raya akifanya kazi kubwa langoni mpaka pale dakika ya 90+7 John Stones alipoisawazishia City goli.
Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili huku Arsenal wakionesha ubora mkubwa kwenye kuzuia licha ya kucheza pungu kwa dakika zaidi ya 45 dhidi ya Manchester City lakini wakaruhusu goli moja pekee, Msimamo mpaka sasa ni Man City wapo kileleni kwa alama 13 huku Arsenal wakiwa nafasi ya nne na alama zao 11.
This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.
Strictly Necessary Cookies
Strictly Necessary Cookie should be enabled at all times so that we can save your preferences for cookie settings.
If you disable this cookie, we will not be able to save your preferences. This means that every time you visit this website you will need to enable or disable cookies again.